Alhamisi 17 Septemba 2026 - 00:15
Viongozi wa Harakati ya Amal na Hizbullah wathibitisha umuhimu wa ushiriki wa kitaifa na ulazima wa Serikali ya Lebanon kubeba majukumu

Hawza/ Viongozi wa Hizbullah na Harakati ya Amal wamefanya mkutano ambapo walijadili maendeleo na matukio ya hivi karibuni nchini Lebanon.

Kwa mujibu wa Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, viongozi wa Hizbullah na Harakati ya Amal — wakiwakilishwa na Sheikh Ali Daamoush, Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Hizbullah, na Dkt. Mustafa Foa’ani, Mwenyekiti wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Amal — wamefanya mkutano ambapo walijadili maendeleo na matukio ya hivi karibuni nchini Lebanon. Majadiliano hayo yalifanyika kwa kuzingatia hali nyeti na tata ambayo Lebanon inapitia, pamoja na changamoto za kisiasa, kitaifa, kiuchumi na kijamii zinazosababishwa na hali hiyo.

Viongozi wa harakati hizo mbili walijikita katika masuala na majukumu kadhaa, yaliyopewa kipaumbele kuimarisha hali ya ndani, kulinda amani ya kiraia, kukabiliana na madhara ya hatua hii, kuharakisha mchakato wa ujenzi upya na kuhakikisha wananchi wanarejea katika vijiji na miji yao, sambamba na kutafuta namna za kushughulikia hali ya kiuchumi, kijamii na kimaisha.

Aidha, mapendekezo kadhaa na hatua za kiutendaji zenye uwezo wa kuendana na hatua hii na kushughulikia masuala yaliyopo yaliwasilishwa, na tamko lifuatalo likatolewa:

Kwanza: Viongozi wa harakati hizo mbili walisisitiza kwamba ushirikiano wa kitaifa na kuishi pamoja kwa mshikamano ni msingi muhimu wa kuilinda Lebanon, na wakakataa kila mtazamo wa kisiasa unaojengwa juu ya kutenga na kuwaondoa wengine, au kutafuta kutawala, au kulazimisha matukio. Aidha, waliwataka wote kuhakikisha kwamba tofauti na kinyongo vinabaki ndani ya mfumo wake wa kisiasa na kikatiba; mfumo unaolinda maslahi ya Walebanon na kuhifadhi Serikali pamoja na taasisi zake.

Pili: Viongozi wa harakati hizo mbili walieleza kwamba; amani ya kiraia ni mstari mwekundu na ni jukumu la kitaifa na la pamoja, na wakakataa aina zote za uchochezi, kuchochea migawanyiko na kuzusha fitina. Pia walithibitisha kwamba kushughulikia masuala yenye utata hakufanywi kwa lugha ya kuzidisha hali na kuchochea mvutano, bali kwa njia ya mazungumzo, maelewano na kurejea kwenye taasisi; jambo ambalo litazuia kuanguka na kuteleza kuelekea mambo yanayotishia amani ya kiraia na kuongeza mzigo kwa Walebanon.

Tatu: Viongozi wa harakati hizo mbili walisisitiza ulazima wa Serikali kubeba kikamilifu majukumu yake, kwa kuhuisha taasisi na vyombo vyake na kutekeleza wajibu wake kwa raia, pamoja na kufanya kazi kwa umakini katika kutatua migogoro ya kiuchumi, kijamii na kimaisha, na kuweka masuala muhimu kwenye njia ya kushughulikiwa kwa vitendo; jambo ambalo litaimarisha uwezo wa Lebanon katika kukabiliana na majukumu yaliyo mbele yake.

Nne: Viongozi wa harakati hizo mbili wanaamini kwamba ujenzi mpya, kuwafidia wale walioathiriwa na kuhakikisha wananchi wanarejea katika vijiji na miji yao si masuala ya kuahirishwa au yaliyocheleweshwa, bali ni kipaumbele cha kitaifa na jukumu linalostahili kupewa kasi katika utekelezaji wake. Hilo lifanywe kupitia kuhamasisha rasilimali rasmi na za wananchi, kuimarisha nafasi ya Serikali na kutumia aina zote za msaada wa Kiarabu na kimataifa uliopo; misaada ambayo itahakikisha wananchi wanabaki katika ardhi yao na maisha yanarejea katika maeneo yaliyoathiriwa.

Tano: Viongozi wa harakati hizo mbili walitaka nguvu zote za kisiasa kuikabili hatua hii kwa uwajibikaji wa hali ya juu wa kitaifa, kujiepusha na maslahi madogo na finyu pamoja na mitazamo inayoongeza tofauti na mgawanyiko, na kuongeza njia za mawasiliano na uratibu; kwa sababu Lebanon haiwezi kuvumilia kusitishwa kwa shughuli au kuongezeka kwa mvutano, na inahitaji zaidi kuliko wakati mwingine wowote maelewano, kazi ya kuijenga na kuunganisha juhudi.

Viongozi wa harakati hizo mbili walisisitiza kwamba; kuvuka hatua ya sasa kunahitaji utashi mpana wa kisiasa, kuweka mbele maslahi ya kitaifa, na kuhama kutoka katika kusimamia migogoro kuelekea kutatua na kushughulikia mizizi yake, na hivyo kufungua njia kuelekea hatua mpya ambayo kaulimbiu yake ni: kuilinda Lebanon, kuijenga upya, kuhakikisha wananchi wanarejea, na kuimarisha Serikali pamoja na taasisi zake.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha